Hali ya chakula inazidi kuwa mbaya DPRK:Amos

24 Oktoba 2011

Mratibu wa masuala ya kibinadamu na msaada wa dharura wa Umoja wa Mataifa Bi Valarie Amos amesema hali ya chakula inazidi kuwa mbaya katika jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea DPRK. Amesema licha ya mavuno kuwa mazuri bado watu wanajaribu kuishi kwa kula mchanganyiko wa vyakula ambavyo vina lishe duni.

Bi amos amesema amezuru hospitali nchini humo, kituo cha yatima, shamba la jumuiya na masoko katika majimbo mawili na kushuhudia utapia mlo wa hali ya juu na anasema anadhani hali inazidi kuwa mbaya mwaka baada ya mwaka nchini humo. Bi Amos alikuwa anazungumza na waandishi wa habari mjini Seoul Korea Kusini alipokamilisha ziara yake.

(SAUTI YA VALARIE AMOS)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud