Haja ya kushughulikia matatizo ya mmomonyoko wa udongo yasisitizwa kwenye mkutano wa kimataifa

21 Oktoba 2011

Kipindi cha miaka 25 ijayo mmomonyoko wa udongo utapunguza uzalishaji wa chakula kwa takribani asilimia 12 huku idadi ya watu ikiendelea kuongezeka. Onyo hili limetolewa kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kukabiliana na hali ya jangwa yaani COP 10 uliohitimishwa leo Ijumaa mjini Changwon, Korea ya Kusini Korea.

Mwandishi wa radio ya Umoja wa Mataifa aliyekuwa katika mkutano huo Jérôme Longué, amesema kwamba matokeo ya mkutano huo ni kushughulikia matatizo ya mmomonyoko wa udongo na changamoto za kuzalisha chakula kukidhi haja ya idadi kubwa ya watu itakayokuwepo duniani. Ameongeza kuwa matokeo ya mmomonyoko wa udongo yatakuwa na athari za moja kwa moja kwa watu walioathirika na kwa mfumo wa maisha ya viumbe na mimea.

Zaidi ya ekari milioni 12 za ardhi ya kilimo inapotea kila mwaka kutokana na hali ya jangwa. Wakati ardhi ya zalishaji inapungua kuwalisha watu bilioni 9 wanaokadiriwa kuishi duniani ifikapo 2050 kutahitaji ongezeko la asilimia 70 la uzalishaji wa chakula.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter