Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yapeleka misaada kwa shirika la majanga ya dharura nchini Thailand

IOM yapeleka misaada kwa shirika la majanga ya dharura nchini Thailand

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM hii leo linatarajiwa kuwapelea msaada waathiriwa wa mafuriko nchini Thailand, msaada wa gharama ya dola laki tano unaofadhiliwa na shirika la kimataifa la maendeleo la Marekani USAID. Msaada huo unajumuisha mashua mbili, mashine 10 za kuondoa maji na jenereta 10.

IOM inafanya jitihada za kupata mashua zaidi ili kuisadia Thailand kukabiliana na janga hilo. Kwa sasa serikali na wenyeji wanafanya jitiahada za kuondoa na kuyaelekeza maji kwenye ghuba ya Thailand. Jumbe Omar Jumbe anafahamisha zaidi.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)