Vikosi vya Kenya vyapambana na Al shabaab nchini Somalia

21 Oktoba 2011

Vikosi vya Kenya kwa sasa viko nchini Somalia kupambana na wanamgambo wa Al Shabaab ambao mara kwa mara wamekuwa wakivuka mpaka na kuingia nchini Kenya ambapo wanatekeleza vitendo vikiwemo vya utekaji nyara na mauaji. Akithibitisha hayo mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga amesema kuwa idadi kubwa ya vikosi vya Kenya iko Somalia kukabiliana na wanamgambo wa Al Shabaab.

(SAUTI YA AUGUSTINE MAHIGA)

Mahiga pia amesema kuwa pande zote mbili za Kenya na Somalia zimekubaliana kupelekwa kwa vikosi vya Kenya nchini Somalia ukiwemo pia uungwaji mkono wa kimataifa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter