Kifo cha Gaddafi kitaleta utulivu Libya:Pillay

21 Oktoba 2011

Mkuu wa haki zabinadamu kwenye Umoja wa mataifa Navi Pillay amesema kuwa kifo cha Muammar Gaddafi na kutekwa kwa miji ya Sirte na Bani Walid ndio mwisho wa ghasia ambazo zimedumu kwa muda wa miezi minane na mateso kwa watu wa Libya.

Pillay amesema kuwa awamu nyingine mpya imeanza ambao itayajali maslahi ya wananchi, kuleta demokrasia na haki za binadamu. Amesema kuwa maelfu ya waathiriwa wa wale waliopoteza maisha, waliotoweka na kuteswa pamoja na waliopitia mateso ya kila aina tangu kuanza kwa ghasia hizo wana haki ya kujua ukweli kulingana na anavyosema Rupert Colville.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter