UM wathibitisha vikosi vya Kenya kuingia Somalia

UM wathibitisha vikosi vya Kenya kuingia Somalia

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augstine Mahiga leo amethibitisha kwamba vikosi vya jeshi la Kenya vimeingia Somalia.

Balozi Mahiga amesema amezungumza na maafisa wa Kenya na Somalia kuhusu hatua hiyo ambayo Kenya inasema imechukua kwa ajili ya usalama na  kukabili uhalifu unaoendeshwa na kundi la wanamgambo wa Kiislam la Al-shabaab.

 Wanamgambo wa kundi hilo wamekuwa wakiendesha vitendo vya tekaji kwa baadhi ya watalii raia wa kigeni nchini Kenya na hivi karibuni waliwateka wafanyakazi wa misaada kwenye kambi kubwa kabisa ya wakimbizi wa Kisomali ya Dadaab iliyoko Kaskazini mwa Kenya.

Balozi Mahiga amesema hatua hiyo ya Kenya haijakika sheria za Umoja wa Mataifa. Amezungumza hayo na mwandishi wa Radio ya Umoja wa Mataifa Jason Nyakundi.

(MAHOJIANO NA BALOZI MAHIGA)