Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Adha kwa watoto wa kipalestina kutokana na kukaliwa imalizwe

Adha kwa watoto wa kipalestina kutokana na kukaliwa imalizwe

Mwakilishi maalmu wa Umoja wa Mataifa kwa hali ya haki za binadamu kwenye himaya ya Palestina Richard Falk ameitaka serikali ya Israel kufuata muongozo wa kuwalinda watoto wa Palestina wanaoishi katika maeneo yanayokaliwa ambao hukamatwa na kushikiliwa. Ameitaka serikali hiyo kuzingatia sheria na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu.

Akizungumza Alhamisi kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapa New York ameonya kwamba kukaliwa kwa Palestina kunadumaza maendeleo ya watoto kutokana na kunyimwa haki kuna athiri afya zao, elimu na usalama kwa ujumla.