Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Familia 24,000 zinaendeshwa na watoto Msumbiji:UNICEF

Familia 24,000 zinaendeshwa na watoto Msumbiji:UNICEF

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema familia zipatazo 24,000 nchini Msumbiji ni za watoto pekeyao. Kwa mujibu wa shirika hilo watoto wengi kati ya hao ambao wamepoteza wazazi wote kutokana na ukimwi huachwa bila msaada wowote .

Lakini sasa kuna shinikizo kubwa kutoka UNICEF na jamii kwa ujumla ya kutaka familia hizo zinazoongozwa na watoto kupewa msaada na serikali. Akizungumza na idhaa hii mku wa kitengo cha kulinda watoto cha UNICEF nchini Msumbiji Mayke Huijbregths (Hi-Brisht) amefafanua kwa nini kuna familia nyingi zinazoongozwa na watoto nchini humo.

(SAUTI YA MAYKE HUIJBREGTHS)