Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA yataka misaada zaidi kwa wakimbizi nchini Ivory Coast

OCHA yataka misaada zaidi kwa wakimbizi nchini Ivory Coast

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema kuwa fedha zaidi zinahitajika ili kugharamia misaada kwa maelfu yawakimbizi nchini Ivoyr Coast. OCHA sasa inatoa wito wa kutolewa kwa misaada ya kuwasaidia wakimbizi kurudi makwao na kuanza upya maisha yao.

Kulingana na OCHA hadi sasa kuna zaidi ya wakimbizi wa ndani 194,000 nchini Ivory Coast huku 25,000 wakiishi kwenye kambi. Hadi sasa ni dola milioni 91 zimetolewa kati ya ombi la dola milioni 292 lililotolewa.