Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban na Bi Karman wajadili haki za binadamu nchini Yemen

Ban na Bi Karman wajadili haki za binadamu nchini Yemen

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amefanya mkutano na mwandishi wa habari na mwanaharakati ambaye ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu raia wa Yemen Tawakkul Karman na kujadili masuala ya haki za binadamu na kudorora kwa masauala ya kibinadamu na uchumi nchini mwake. Wakati wa mkutano huo uliofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Ban na Bi Karman walibadilishana mawazo kuhusu hali ilivyo kwa sasa nchini Yemen hasa kuongezeka kwa ghasia. Ban alimhakikishia Karman kuwa Umoja wa Mataifa unafanya kila uwezalo kuwasaidia watu nchini Yemen kutatua mzozo ulio nchini mwao.