Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC yaitaka Malawi kueleza sababu ya kutomkamata rais Bashir

ICC yaitaka Malawi kueleza sababu ya kutomkamata rais Bashir

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya Hague imeitaka Malawi kueleza sababu zilizoifanya kutomkamata rais wa Sudan Omar Hassan al- Bashir ambaye anatafutwa na mahakama hiyo kutokana na mashataka ya uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki baada ya ripoti kuwa alifanya ziara nchini Malawi.

Haya yanajiri baada ya ripoti za vyombo vya habari kusema kuwa rais Bashir aliitembelea malawi siku ya Ijumaa. Mwaka uliopita mahakama ya ICC ilitangaza waranti wa pili wa kukamatwa kwa rais Bashir baada ya kumuongezea shtaka la mauaji ya halaiki kwenye orodha ya mashtaka yanayomkabili.