Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Myanmar bado inaendelea kukandamiza haki za binadamu-UM

Myanmar bado inaendelea kukandamiza haki za binadamu-UM

Myanmar ikiwa imepiga hatua kubwa pamoja na kupunguza mbinyo kwa vyombo vya habari na kupewa nafasi kwa vyama vya siasa, hata hivyo kwa kiasi kikubwa Myanmar inaendelea kuziendea kinyume haki za binadamu. Hayo ni kwa mujibu wa mtaalamu mmoja wa Umoja wa Mataifa ambaye amelitaka taifa hilo kufanya haraka ili kuwaachia huru wafungwa kadhaa wa kisiasa wanaoendelea kusota gerezani.

Mtaalamu huyo Tomás Ojea Quintana ambaye alikuwa akizungumza kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amesema kuwa bado kunaendelea kujiri ripoti za uvunjifu wa haki za binadamu.

Amezitaka mamlaka za dola kufufua mifumo yenye kuzingatia haki na ukweli pamoja kuondoa mazingira yote yanayokwaza ustawi wa haki za binadamu.