Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya kirai yataka ukomeshwaji uporaji wa ardhi

Mashirika ya kirai yataka ukomeshwaji uporaji wa ardhi

Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa unaojadilia hali ya ukame, yametaka ukomeshwaji mienendo wa upokaji ardhi unaendelea kufanywa katika mataifa kadhaa.

Mashirika hayo ambayo yanakutana katika mji wa Changwon, Korea Kusini yamesema kuwa pamoja vitendo vya uchukuaji ardhi vinavyopaliliwa na baadhi ya tawala za kidola na makundi ya kibiashara havipaswi kuendelea kuungwa mkono hasa katika wakati huu ambao baadhi ya maeneo yameanza kuonja joto la jangwa. Inakadiriwa kuwa kiasi cha hekali milioni 227 ambacho kilikuwa kikimilikiwa na jamii za kawaida za zile za kizawa, kimetolewa kwa wawekezaji wa kimataifa.

Mwenendo huo unatajwa kushamiri zaidi barani Afrika na kwa mujibu wa takwimu, utoaji leseni huo hufanywa katika hali ya usili mkubwa.