Mwanakandanda maarufu wa Brazili aelimisha vijana kuhusu Ukimwi

20 Oktoba 2011

Ronaldo de Assis Moreira mwanasoka maarufu kutoka nchini Brazili ambaye pia anajulikana kama Ronaldinho amekubali mwaliko kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS na wizara ya afya ya Brazil kuchagiza vita dhidi ya ukimwi kwa kutumia michezo.

Mkurugenzi mkuu wa UNAIDS Michel Sidibe amesema Ronaldinho anamvuto mkubwa miongoni mwa vijana duniani kote na sauti yake itawafikia mamilioni ya watu na kuongeza nguvu mpya katika lengo la Umoja wa Mataifa la kufikia maambukizi mapya sufuri ya HIV.

Nayo wizara ya afya ya Brazili imesema kutokana na ujuzi wake wa muda mrefu katika kandanda bwana Moreira au Ronaldinho atatumia michezo kama njia ya kuwahusisha vijana na kuwaelimisha kuhusu ugonjwa wa ukimwi.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter