Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msafara wa wahamiaji wa Afrika kutoka Libya umewasili Chad:IOM

Msafara wa wahamiaji wa Afrika kutoka Libya umewasili Chad:IOM

Zaidi ya wahamiaji 1220 kutoka nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara waliohamishwa kutoka mjini Sebha Kusini mwa Libya wiki mbili zilizopita sasa wamewasili Chad baada ya safari ndefu.

Wahamiaji hao walisafirishwa kwa msafara wa malori 15 kutoka kwenye kituo cha shirika la kimataifa la uhamiaji IOM mjini Sebha kwa msaada wa shirika hilo. Kuwasili kwao kumekuja wakati IOM inajiandaa kusafirisha kundi lingine kubwa la wahamiaji linalosubiri mjini Sebha. Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM anafafanua kuhusu kuwasili kwao.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)