Kanali Muammar Gaddafi ameuawa

20 Oktoba 2011

Baraza la mpito la Libya NTC limesema aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi ameuawa leo mjini Sirte. Taarifa za kifo hicho zimetolewa baada ya majeshi ya Baraza la Mpito kutangaza yanaudhibiti mji wa Sirte, mji alikozaliwa kiongozi huyo. Kwa mujibu wa afisa wa Baraza la Mpito Abdel Majid kiongozi huyo alikamatwa na kujeruhiwa miguu yake yote miwili na kubebwa na gari la wagonjwa kupelekwa Misrata.

Akizungumzia kifo hicho na mambo yanyoendelea Libya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Gaddafi alichuka madaraka Libya mwaka 1969 na hivyo kuwa madarakani kwa miaka 42, alitolewa madarakani katika machafuko yaliyozuka mwezi Februari. Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC ilitoa kibali cha Gadafi kukamatwa kutokana na madai ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter