Skip to main content

UM kuimarisha jamii zinazoishi katika maeneo makavu

UM kuimarisha jamii zinazoishi katika maeneo makavu

Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP inasema kuongeza uwekezaji katika maeneo makavu, kuimarisha uhusiano baina ya sayansi na sera na maisha mchanganyiko kwa jamii ili kupunguza shinikizo kwa mali asili ni miongoni mwa suluhu ya kutambua umuhimu wa maeneo makavu.

Ripoti hiyo ya UNEP iitwayo 'Global Drylands: A UN System-wide response' imeainisha mtazamo wa pamoja na ajenda za Umoja wa Mataifa za kudhibiti maeneo makavu, jukumu lake katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na usalama wa chakula kupitia maendeleo na mtazamo wa uwekezaji.

UNEP inasema matumizi mabaya ya ardhi na maji ndio sababu kubwa ya mmomonyoko wa ardhi, jangwa,misitu, mbuga za savannah na maeneo makavu ambayo yanachukua asilimia 40 ya ardhi ya dunia ambayo inasaidia watu takribani bilioni 2 na asilimia 90 ya watu hao wanaishi katika nchi zinazoendelea.