Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yaitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia Somali

Tanzania yaitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia Somali

Serikali ya Tanzania leo imeitolea wito jumuiya ya kimataifa kutolipa kisogo eneo la Pembe ya Afrika ambalo wakati huu inaandamwa na hali ngumu ya ukosefu wa chakula na kusababisha wimbi kubwa la wakimbizi kutorokea katika nchi za jirani.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje Bwana Bernad Memba ambaye amesema jumuiya za kimataifa hazipaswi kukaa kimya zinawajibika kunyosha mikono ili kunusuru maisha ya mamilioni ya watu wanaoendelea kutaabika huko Somalia.

Waziri Membe alikuwa akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mdahalo ulioangazia nafasi ya Umoja wa Mataifa na mafungamano ya kimataifa.

(SAUTI YA BERNAD MEMBE)