Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matatizo yanayoikabili pembe ya Afrika bado ni makubwa:UNICEF

Matatizo yanayoikabili pembe ya Afrika bado ni makubwa:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema msaada wa kimataifa kuokoa maisha ya watoto kwenye Pembe ya Afrika unaonyesha matumaini lakini bado juhudi zaidi zinahitajika ili kuokoa maisha ya maelfu ya watoto walioko kwenye hatari ya kufa na utapiamlo na magonjwa mengine.

UNICEF imeyasema hayo katika ripoti yake inayoelezea hatua zilizopigwa miezi mitatu baada ya janga la njaa kutangazwa Pembe ya Afrika. Kwa mujibu wa mkurugenzi wa UNICEF wa kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Elhadj As Sy maisha ya watoto wengi yameokolewa Somalia, kwenye kambi za wakimbizi katika nchi jirani na nchi za Kenya, Ethiopia na Djibouti. Jason Nyakundi anaarifuu

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)