Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Baraza Kuu la UM ahofia waathirika wa mafuriko Thailand, Cambodia na nchi zingine za Kusini Mashariki mwa Asia:

Rais wa Baraza Kuu la UM ahofia waathirika wa mafuriko Thailand, Cambodia na nchi zingine za Kusini Mashariki mwa Asia:

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser, ameelezea hofu, huruma na huzuni yake kufuatia kupotea kwa maisha ya mamia ya watu nchini Thailand, Cambodia na nchi za jirani za Kusini Mashariki mwa Asia kutokana na mafuriko.

Hivi sasa inakadiriwa kwamba mafuriko hayo yameshakatili maisha ya mamia na kuwacha mamilioni wakikosa makazi hususani Thailand, Cambodia, Laos, Ufilipino na Viet Nam.

Rais huyo Al-Nasser ameyapongeza mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa, mifuko ya hisani na programu mbalimbali zilizoandaliwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ambao wamejitolea msaada unaohitajika kusaidia jamii na nchi zilizoathirika.

Nasser amesema kuimarisha njia za kujikinga na majanga ya asili itasalia kuwa ajenda ya Baraza Kuu la 66 na amezitaka nchi zote wanachama kujitahidi kuzielimisha na kuzisaidia jamii zao kujikinga na majanga.