Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za Asia-Pacific na jumuiya za kijamii wakutana katika maandalizi ya RIO+20

Nchi za Asia-Pacific na jumuiya za kijamii wakutana katika maandalizi ya RIO+20

Zaidi ya wajumbe wa serikali na jumuiya za kijamii 250 kutoka mataifa zaidi ya 40 ya Asia-Pacific wamekutana leo mjini Seoul Korea ili kuafikiana msimamo na taarifa ya kikanda itakayowasilishwa kwenye mkutano wa Umoja wa mataifa kuhusu maendeleo endelevu (UNCSD) ambao pia hujulikana kama Rio + 20 unaotarajiwa kufanyika kwakani.

Mkutano huo unaandaa tamko la kikanda ambalo litatoa mtazamo wa eneo hilo, masuala wanayoyapa kipaumbele, na kbainisha mikakati maalumu ya utekelezaji wa Rio + 20. Mkutano huo pia unajadili mada mbili za mkutano wa Rio+20 ambazo ni uchumi unaojali mazingira kwa ajili ya maendeleo endelevu na kutokomeza umasikini, na pili mfumo maalumu kwa ajili ya utekelezaji wa maendeleo endelevu.  …. mmoja wa wanaohudhuria mkutano huo.

(SAUTI YA )