Mashirika ya UM yajitolea kuinua wanawake wa vijijini

Mashirika ya UM yajitolea kuinua wanawake wa vijijini

Wakuu wawili wa mashirika ya Umoja wa Mataifa akiwemo Michelle Bachelet mkurugenzi wa idara ya Umoja wa mataifa inayohusika na usawa wa kijinsia(UN WOMEN) na Kanayo Nwanze aliye rais wa mfuko wa kilimo wa kimataifa IFAD wamekubalina kushirikiana katika kuwanua wanawake wa vijijini kwa kuwekeza kwenye kilimo, uchumi na kwenye masuala ya usalama.

Wakiwa mjini Rome wawili hao walijadili njia ambazo mashirika yao yanaweza kushirikiana katika kuinua maisha ya wanawake wa vijijini na kuwawezesha kufanya maamuzi kama njia ya kumaliza umaskini. Bi Bachelet ambaye ni rais wa zamani wa Chile amekuwa kwenye mstari wa mbele kupigia debe uwekezaji kwa wanawake wa vijiji tangu achukue wadhifa wake mwaka uliopita.