Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wamtunuku Maya Angelou

UM wamtunuku Maya Angelou

Mshairi na mwandishi wa Kimarekani Maya Angelou ametunukiwa heshima na Umoja wa Mataifa kama mmoja wa wazee wa busara wa jamii ya wanazuoni mahiri na watetezi wa haki za binadamu na za jamii.

Mwaka 2011 umetangazwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa ni mwaka wa kimataifa wa watu wenye asili ya Afrika kwa kutambua mchango wao mkubwa katika jumuiya ya kimataifa. Bi Angelou ni miongoni mwa watu wenye asili ya Afrika ambao wataonyesha sanaa na utamaduni wa Kiafrika kwenye maonesho maalumu yatakayofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Bi Angelou ataonesha shairi liitwalo “Brave and startling Truth” aliloliandika maalumu kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Mataifa