Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali zatakiwa kutambua uhamiaji kama suala la kubaini hali ya kiafya

Serikali zatakiwa kutambua uhamiaji kama suala la kubaini hali ya kiafya

Huku wajumbe kutoka mataifa mbali mbali wakikusanyika mjini Rio de Janeiro kwenye mkutano wa kwanza kabisa kuhusu masuala ya kijamii kwenye afya, shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limezitaka serikali kutambua suala la uhamiaji kama suala linalobainisha afya ya wahamiaji. Mkurugenzi mkuu wa IOM William Lacy Swing amesema kuwa inahitaji kukubalika kuwa wakati wahamiaji wanapochangia kwenye ukuaji wa uchumi wa kitaifa na kimataifa huwa wanapitia hali hizi wanapohama suala linalochongia wao kuathirika kiafya. Jumbe Omari Jumbe kutoka IOM anaeleza.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE )