Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji nchini Yemen

UM walaani matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji nchini Yemen

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani mauaji ya waandamanaji wenye amani kwenye miji ya sanaa na Taiz nchini Yemen. Ghasia zilizuka mwishoni mwa juma na ofisi hiyo ya haki za binadamu inasema kuwa mauaji hayo yalitokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi kutoka kwa vikosi vya usalama. Hata hivyo ghasia zinaendelea kushuhudiwa wakati waandamanaji wanapotaka uongozi wa rais Ali Abdullah Saleh wa miaka 33 uondoke madarakani. Rupert Colville ambaye ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya UM amelaani pia vikali mauaji hayo.

(SAUTI YA RUPERT COLVILE)