Waomba hifadhi kwenda nchi zilizostawi waongezeka

18 Oktoba 2011

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa nchi zilizostawi zimeshuhudia kuongezeka kwa asilimia 17 watu wanaoomba hifadhi wakati wa nusu ya kwanza ya mwaka ambapo idadi kubwa ya maombi ya hifadhi inapotoka kwenye nchi zilizo na mizozo ya muda mrefu. Kulingana na ripoti ya UNHCR maombi 198,300 yalitumwa kati ya mwezi Januari na mwezi Juni mwaka huu ikilinganishwa na maombi 169,000 kwenye kipindi kama hicho mwaka uliopita. UNHCR inatabiri idadi ya maombi kufikia maombi 420,000 itimiapo mwishoni mwa mwaka huu. Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud