Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aelezea mafanikio yaliyopo katika ubadilishanaji wa wafungwa kwenye eneo la mashariki ya kati

Ban aelezea mafanikio yaliyopo katika ubadilishanaji wa wafungwa kwenye eneo la mashariki ya kati

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anaamini kuwa kubadilishana wafungwa kati ya Israeal na Palestina kutaleta matokeo mema kwenye mpango wa amani wa mashariki ya kati uliokwama.

Ban amesema kuwa amefurahishwa na shughuli ya kubadilishana wafungwa baada ya miaka mingi ya majadiliano. UM umekuwa ukitoa wito wa kuachiliwa kwa Gilad Shalit na wapalestina wote ambao haki zao zimekiukwa.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Shalit kwanza alichukuliwa ukanda wa Gaza na kupelekwa Misri, ambapo alikabidhiwa kwa maafisa wa Israeli na baadaye kuvuka mipaka. Zaidi ya Wapalestina 1,000 wanatarajiwa kuachiliwa huru katika mpango wa kubadilishana wafungwa baina ya Israeli na Hamas. Wafungwa wa mwanzo 477 wameachiliwa huru leo Jumanne. Shalit alitekwa mwaka 2006 na wapiganaji wa Hamas walioingia Israeli.