Skip to main content

Mkuu wa OCHA aelezea hofu ya mafuriko kusini mashariki mwa Asia

Mkuu wa OCHA aelezea hofu ya mafuriko kusini mashariki mwa Asia

Mkuu wa masuala ya kibinadamu na msaada wa dharura wa Umoja wa Mataifa ameelezea hofu yake kuhusu kuongezeka kwa athari za mafuriko kwa mamilioni ya watu Kusini Mashariki mwa Asia. Bi Valarie Amos ambaye yuko ziarani katika eneo hilo amesema hali inatarajiwa kuwa mbaya zaidi wakati vina vya maji vya mito vikiongezeka na mvua bado zinanyesha.

Amesema mafuriko makubwa yamekatili maisha ya watu zaidi ya 700 nchini Cambodia na Thailand, wakati Laos, Ufilipino na Viet Nam, nyumba, mazao na miundombinu imeharibiwa vibaya na mafuriko na kuwaacha mamilioni ya watu bila makazi na hofu ya kupoteza kila kitu. Amesema Umoja wa Mataifa na washirika wake wako tayari kutoa msaada kwa mipango ya serikali ya kuwanusuru watu walioathirika.