Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano zaidi watakiwa kukabili hali ya jangwa:UM

Ushirikiano zaidi watakiwa kukabili hali ya jangwa:UM

Hali ya jangwa inaathiri takribani watu bilioni moja kote duniani kila mwaka na asilimia moja ya ardhi yenye rutuba hupotea. Kutokana na hali hiyo Umoja wa Mataifa kupitia mkataba wake wa kupambana na jangwa COP unaendesha mkutano kwa wiki mbili nchini Korea Kusini.

Mkutano huo ulioanza leo unajadili jinsi ya kupambana na hali ya jangwa na ukame na umewaleta pamoja mawaziri 40 kutoka nchi mbalimbali, viongozi wa serikali, mashirika ya kimataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohusika na masuala ya mazingira. Kwa niaba ya Umoja wa Mataifa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulazizi Al-Nasser amesema ushirikiano na mshikamano unahitajika ili kumaliza tatizo la jangwa, mmomonyoko wa udongo na ukame. Ametoa wito kwa serikali zote pia kulitilia maanani suala la usalama wa chakula na kupigia upatu uchumi unaojali mazingira.