Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ajionea kupungua kwa theluji nchini Uswisi

Ban ajionea kupungua kwa theluji nchini Uswisi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alijionea mwenyewe akitumia ndege aina ya helkopta kupungua kwa theluji kwenye mji wa Bern nchini uswisi na baadaye kujadiliana na rais Micheline Calmy- Rey kuhusu maendeleo na mkutano wa UM kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa utakaoandaliwa nchini Afrika Kusini.

Akiwa nchini Uswisi ambapo alihudhuria kikao cha chama cha wabunge Ban alikutana na wabunge kadha wa bunge la Australia akiwemo spika Harry Jenkins ambapo walijadili masuala kadha yakiwemo hatua zilizopigwa kuelekea kutimizwa kwa malengo ya maendeleo ya milenia.