Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mpango wa Isreal kuanzisha ujenzi wa makazi Jerusalem

Ban alaani mpango wa Isreal kuanzisha ujenzi wa makazi Jerusalem

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameonyesha wasiwasi wake kufuatia tangazo la serikali ya Israel la kutaka kuweka makazi mapya ya majengo katika eneo inalokalia kwa nguvu la Jerusalame Mashariki akisema kuwa kitendo hicho ni sawa na kukaribisha machafuko.

Ban amesema kuwa juhudi zozote za kutaka kuendeleza makazi hayo ni hatua isiyokubalika hasa wakati huu kunakofanyika mipango wa urejeshwaji mezani majadiliano ya kusaka amani kwa pande zote ambayo yalivunjika hivi karibuni. Mpango huo unakusudiwa kuchukuliwa na Israel wa kuweka makazi mapya kwenye eneo hilo, ni hatua ambayo pia inakwenda kinyume na mwito uliotolewa na pande nne zinazofuatilia mzozo huo ambazo zinapendekeza usitishwaji wa ujenzi huo.

Pande hizo nne zinazojumuisha Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Russia na Marekani zimeweka zingatio la wazi likitaka kusitishwa ujenzi wa makazi hayo.