Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Changamoto kubwa hii leo ni upungufu wa imani:Ban

Changamoto kubwa hii leo ni upungufu wa imani:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema serikali zote duniani zinakabiliwa na shinikizo kubwa la kukabiliana na matatizo ya bajeti kutokana na kuyumba kwa uchumi, lakini amesisitiza changamoto kubwa zaidi sio upungufu wa rasilimali bali ni upungufu wa imani.

Ban ameyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa muungano wa wabunge IPU mjini Berne Switzeland. Ameongeza kuwa watu wanapoteza imani kwa serikali na taasisi zao kwa kutofanya yanayotakiwa. Ban amesema  ili kuondoa pengo hilo la kukosa imani hatua za pamoja zinahitajika, hatua ambazo zitaonyesha hali halisi ya changamoto zinazoikabilia dunia kwa sasa.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Pia amejadili masuala mengine mbalimbali na IPu ikiwemo mabadiliko yanayoendelea katika ulimwengu wa Kiarabu, msukumo wa kufikia malengo ya maendeleo ya milenia, mkutano ujao wa Rio+20, matatizo ya kiuchumi yanayoendelea, hasa hali barani Ulaya na masuala ya amani na usalama duniani.