Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za kupambana na upofu nchini Kenya

Juhudi za kupambana na upofu nchini Kenya

 

Makala yetu ya wiki hii inaangazia siku ya kuona duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka alhamisi ya pili ya mwezi Oktoba. Shirika la afya duniani WHO limesema katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuona kwamba mkazo wa kimataifa unapaswa kuelekezwa katika kupunguza upofu, matatizo ya kutoona mbali au karibu na kuwasaidia wasioona.

Maadhimisho ya mwaka huu pia ni ya kuchagiza malengo ya 2020 ya kuhakikisha matatizo ya kutoona yamepungzwa na kutokomezwa yaani “vision 2020” haki ya kuona” juhudi ambazo zimeanzishwa na WHO na shirika la kimataifa la kuzuia upofu. Mwandishi wetu kutoka Nairobi Jason Nyakundi ametuandalia makala kuhusu tatizo la upofu nchini Kenya. Ungana naye.