Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka nchi zinazoendelea kuongeza kasi juu ya mipango ya afya kwa wanawake na watoto

Ban ataka nchi zinazoendelea kuongeza kasi juu ya mipango ya afya kwa wanawake na watoto

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezitaka nchi zinazoendelea kutopoteza mwelekeo wa kushughulikia vipaumbele vya afya za wanawake na watoto akionya kuwa kuna kazi kubwa inayopaswa kufanywa mbeleni.

 Akizungumza kwenye hafla ya ushirikiano wa Kusin-Kusin Mjini New York Ban amesema kuwa ametia moyo sana na hatua zilizopigwa na nchi hizo tangu kuanzishwa kwa wakfu maalumu unaoshughulikia afya za wanawake na watoto.

Hata hivyo amesema kuwa nchi zinazoendelea zinapaswa kuendelea kusuma mbele maendeleo hayo yanayofikia sasa na kuonya kile alichosema kubadilisha mwelekeo.

Mpango huo wa kimataifa umetanga zaidi ya dola za kimarekani bilioni 40 kwa ajili ya utekelezaji miradi inayojali afya za wanawake na watoto