Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikosi vya kulinda amani vinahitaji usalama zaidi- UM

Vikosi vya kulinda amani vinahitaji usalama zaidi- UM

Mkuu mpya wa kamandi ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa amezungumzia umuhimu wa watendakazi kwenye vikosi hivyo kuhakikishiwa usalama wa maisha wao pindi wanawajibika.

Umoja wa Mataifa unajumla ya maafisa 120,000 wanaofanya kazi za ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, mkuu huyo mpya Hervé Ladsous,amesema kuwa tukio la hapo majuzi la kuuliwa kwa walinzi watatu wa amani huko Darfur , Sudan linaanika hali ya mazingira magumu ya kiusalama inayowaandama maafisa hao.

Amesema ni lazima sasa kuwekeza vyakutosha kwenye maeneo ya usalama ili kuepukana na matukio ya kuuliwa kwa maafisa wake wawapo kwenye majukumu