Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Balozi wa hisani Zidane aenda Mali kujadili umaskini

Balozi wa hisani Zidane aenda Mali kujadili umaskini

Mwanasoka mashuri wa enzi hizo ambaye sasa ni mjumbe wa hisani wa Umoja wa Mataifa Zinédine Zidane,anatazamiwa kuelekea nchini Mali kwa ajili ya kuweka zingatio la kukabiliana na tatizo la umaskini

 Zidane ambaye safari yake imepangwa kufanyika wiki ijayo amesema kuwa anakwenda huko kwa shabaya moja ya kujadilia na kuhimiza mikakati inayoendelea kuchukuliwa ya kukabiliana na umaskini.

 Mwanasoka huyo nyota wa zamani ambaye ni raia wa Ufaransa amesema kuwa jukumu la kukabili umaskini ni la kila mtu.

Amekuwa balozi wa hisani wa shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP kwa miaka 10 sasa.Akiwa nchini Mali anatazamia kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo ile inayoendeshwa na wanawake