Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM na serikali ya Kenya watoa chanjo kwa wakimbizi kutoka Somalia

IOM na serikali ya Kenya watoa chanjo kwa wakimbizi kutoka Somalia

Zaidi ya wakimbizi 2000 wa Kisomali wanaowasili nchini Kenya kupitia kwa mji wa Liboi ulio kwenye mpaka kati ya Kenya na Somalia wamepata chanjo dhidhi ya ugonjwa wa polio na surua kufuatia ushirikiano kati ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na serikali ya Kenya.

IOM na wizara ya afya nchini Kenya walizindua shughuli hiyo ya kutoa chanjo mnamo Oktoba sita mwaka huu kwa wasomali wanaongia nchini Kenya. Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia kuripotiwa kwa visa kadha vya ugonjwa wa polio na surua kwenye sehemu kadhaa mkoani kaskazini mashariki nchini Kenya ambapo maelfu ya wakimbizi kutoka Somalia wamepiga kambi. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)