Pillay ataka jamii ya kimataifa kuchukua hatua nchini Syria

14 Oktoba 2011

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka ili kuwalinda raia nchini Syria ambapo idadi ya waliouawa sasa imefikia watu 3000 wakiwemo watoto 180.

Pillay amesema kuwa tangu kuanza kwa ghasia nchini Syria serikali imekuwa ikitumia nguvu kupita kiasi wakati kuvunja maandamano ya amani. Matumizi ya risasi na mashambulizi ya mabomu kwa makaazi ni kati ya mbinu ambazo zimekuwa zikitumika kwenye miji nchi Syria. Pillay pia amesema kuwa maelfu ya watu wengine wamekamatwa , kufungwa huku wengine wakitoweka na kuteswa. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud