Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wananchi wa Haiti washiriki kikamilifu kusafisha maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko

Wananchi wa Haiti washiriki kikamilifu kusafisha maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko

Mamia kwa maelfu ya wananchi wa Haiti wamejitokeza kushiriki kikamilifu kusafisha masalia ya zaga zaga zilizoachw awakati wa tetemeko la ardhi iliyoikumba nchi hiyo mwaka uliopita.

Taarifa za awali zinasema kuwa tetemeko hilo lililosababisha maafa makubwa limeacha masalia mengi ya taka taka ambazo sasa zimeanza kusafishwa katika mpango unaratibiwa na shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP. Afisa wa shirika hilo nchini Haiti Jessica Faieta, amesema kazi kubwa inafanyika sasa ni kuondoa masalia hayo

Kazi hiyo inafanywa kwa mashirikiano ya pamoja baina ya serikali, mashirika ya kiraia na makundi mengine ya watu wa kawaida.