Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko katika jeshi na polisi ni muhimu katika kuzuia migogoro

Mabadiliko katika jeshi na polisi ni muhimu katika kuzuia migogoro

Kufanyia mabadiliko jeshi na mashirika mengine ya usalama ni muhimu kwa kuzuia kuzuka tena kwa migogoro. Hayo yamesemwa leo na mkuu wa operesheni za kulinda amani wa Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous, wakati Baraza la Usalama lilipokutana kujadili mabadiliko katika sekta ya usalama Afrika.

Akitolea mfano Liberia bwana Ladsous amesema kuwa sababu matatizo ya usalama hayakushughulikiwa ipasavyo katika mwaka 1990 yalichagia kuzuka tena vita na kuporomoka kwa uchumi. Ameongeza kuwa nchi za Afrika zimeanza kutambua kuhusu kushughulikia suala hili.