Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aipongeza Cameroon kwa kuendesha uchaguzi wa amani

Ban aipongeza Cameroon kwa kuendesha uchaguzi wa amani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza Wacameroon kwa kuendesha uchaguzi mkuu wa Rais wa amani na utulivu lakini kushughulikia malalamiko yote yaliyojitokeza.

Uchaguzi huo uliofanyika siku ya Juumapili namuhusisha Rais aliyeko madarakani tangu mwaka 1982 Paul Biya, akichuana na wagombea wengine 22. Katika taarifa yake Ban amezitaka pande zote za siasa kutumia mfumo wa sheria kutatua mivutano iliyojitokeza katika uchaguzi.

Pia ameitaka serikali ya Cameroon kuhakikisha kwamba madai yote yanayohusiana na mchakato wa uchaguzi yanashughulikiwa ipasavyo na kwa uwazi.