Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabalozi wema wa UNAIDS wachagiza vita dhidi ya Ukimwi

Mabalozi wema wa UNAIDS wachagiza vita dhidi ya Ukimwi

Katika siku ya ufunguzi wa kongamano la kimataifa mjini Moscow, Urusi kuhusu lengo namba 6 la maendeleo ya milenia ambalo ni kupambana na ukimwi, malaria na magonjwa mengine, mcheza filamu wa Inda Preity Zinta, mshindi wa kombe la dunia la kandada ya wanawake Lorrie Fair na mwanaharakati wa ukimwi kutoka Urusi Alexander Volgina wakishirikiana na mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS Michel Sidibe wamekuwa na mjadala wa jinsi gani ya kulifanya lengo la milenia namba 6 kutimia.

Jopo hilo ambalo ni la mabalozi wema wa UNAIDS limeelezea umuhimu wa mchango wa mataifa ya BRICS katika vita dhidi ya ukimwi na changamoto zingine za kuwa na kizazi huru bila maambukizi ya HIV.

Nchi za BRICS ni Brazil, Urusi, India, Uchina na Afrika ya Kusini nchi ambazo ni maskani ya asilimia 40 ya watu wanaoishi na virusi vya HIV duniani. Sidibe amesema wakati mataifa hayo yamepiga hatua katika kuzuia maambukizi na matibabu, lengo la watu wote kupata tiba linasalia kuwa changamoto kwa mataifa manne kati ya matano ya BRICS kwani theluthi moja tu ya watu ndio wanaweza kupata dawa za kurefusha maisha.