Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Aisa Kirabo Kacyira kutoka Rwanda ateuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi mtendaji wa UNHABITAT

Aisa Kirabo Kacyira kutoka Rwanda ateuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi mtendaji wa UNHABITAT

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Bi Aisa Kirabo Kacyira kutoka Rwanda kuwa naibu mkurugenzi mtendaji na katibu mkuu msaidizi wa shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UNHABITAT. Bi Kirabo anayechukua nafasi ya Bi Inga Bjork hivi sasa ni gavana wa jimbo la Mashariki ambalo ni jimbo kubwa kabisa nchini Rwanda .

Kabla ya hapo bi Kirabo alikuwa meya wa mji wa Kigali ambapo alifanikisha kuinua kiwango cha safi wa mji huo, kulinda mazingira, usalama na mradi wa nyumba za bei nafu na kuongeza nafasi za ajira mafanikio ambayo yaliufanya mji huo kushinda tuzo ya UNHABITAT mwaka 2008. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKNDI)