Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulimwengu kupata mtu wa bilioni 7 mwishoni mwa mwezi

Ulimwengu kupata mtu wa bilioni 7 mwishoni mwa mwezi

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa ulimwengu unastahili kujitahidi zaidi wakati idadi ya watu duniani inapotimia watu bilioni 7 baadaye mwezi huu. Akihutubia mkutano wa kimataifa kuhusu nishati safi mjini Copenhagen unaowaleta pamoja viongozi wa serikali , biashara na mashirika ya umma Ban amesema kuwa watoto wanaozaliwa ni lazima wapate maisha mema ya baadaye.

Kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa ni kwamba mtu wa bilioni saba duniani atazaliwa mnamo tarehe 31 mwezi huu.