Wajumbe wa Baraza la Haki za binadamu walaumiwa na Syria

12 Oktoba 2011

Ripoti ya tathimini ya hali ya haki za binadamu nchini Syria imepitishwa na Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa lakini si kimya kimya, kwani Syria imewashutumu baadhi ya wajumbe wa baraza hilo kuingiza siasa katika tathimini hiyo.

Tathimini hiyo ya Syria ni sehemu ya muendelezo wa tathimini inayoendelea kupitia utekelezaji wa hali za haki za binadamu kwa nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa. Kamishina mkuu wa haki za binadamu wiki iliyopita alisema watu 2900 wameuawa Syria tangu kuanza kwa maandamano ya kutaka demokrasia mwaka huu.

Faysal Mekdad naibu waziri wa mambo ya nje wa Syria amekaribisha tathimini hiyo lakini amesema mchakato haukufanyika kama ilivyopaswa.

(SAUTI YA FAYSAL MEKDAD)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter