Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uzalishaji wa Kasumba waongezeka Afghanistan:UNODC

Uzalishaji wa Kasumba waongezeka Afghanistan:UNODC

Uzalishaji wa kasumba umeongezeka kwa asilimia 60 nchini Afghanistan kwa mwaka huu. Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa na serikali ya Afghanistan.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uhalifu na Madawa UNODC inasema kilimo cha kasumba nchini humo kimeongezeka kwa asilimia 7 mwaka 2011 kutokana na usalama mdogo, matatizo ya kiuchumi na kupanda kwa bei ya zao hilo.

 Afghanistan inazalisha karibu asilimia 80 ya kasumba yote duniani na nyingi inalimwa kwenye majimbo yenye machafuko ya Helmand na Kandahar. Hivi sasa majimbo 17 kati ya 34 ya nchi hiyo yanazalisha kasumba ikiwa ni majimbo matatu zaidi ikilinganishwa na 14 yaliyokuwa yakilima mwaka jana.

Kwa mujibu wa UNODC hali hii inadhihirisha uhusiano uliopo baina ya ukosefu wa usalama na kilimo cha kasumba nchini humo.