Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kurejea nyumbani kwa wakimbizi wa Sri Lanka kungo’a nanga

Kurejea nyumbani kwa wakimbizi wa Sri Lanka kungo’a nanga

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Linatarjia kupokea kundi la kwanza la wakimbizi raia wa Sri Lanka watakaosafiri kwa mashua kutoka nchini India hapo kesho kwenye mpango unaoungwa mkono na Sri Lanka pamoja na India. Hadi sasa wakimbizi wote wa Sri Lanka wamekuwa wakirejea nyumbani kwa njia ya ndege.

Watakaorejea nyumbani ni watu 37 wanaowakilisha familia 15. Tangu kuisha kwa mzozo May mwaka 2009 wakimbizi wa Sri Lanka wamekuwa wakirejea nyumbani kutoka India na wengine wachache kutoka nchi zingine.