Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OHCHR yahuzunishwa na kunyongwa kwa watu nchini Saudi Arabia

OHCHR yahuzunishwa na kunyongwa kwa watu nchini Saudi Arabia

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imehusunishwa na hatua ya Saudi Arabia ya siku ya ijumaa ya kuwanyonga hadharani wanaume 15, 8 kati yao wakiwa ni wahamiaji wafanyikazi raia wa kigeni. Ofisi ya haki za binadamu ya UM inasema kuwa kati ya watu 58 walioripotiwa kunyongwa nchini Saudi Arabia mwaka huu 20 kati yao walikuwa ni wahamiaji wafanyikazi wa kigeni.

Ofisi hiyo kwa sasa inatoa i wito kwa Saudi Arabia kujiunga na mataifa 140 yaliyopiga marufuku hukumu ya kifo.