Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa kipindupindu waua watu Afrika Magharibi

Ugonjwa wa kipindupindu waua watu Afrika Magharibi

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa kuna zaidi ya visa 85,000 kipindupindu Magharibi na kati kati mwa Afrika hasa nchini Chad, Cameroon na Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Hali hiyo inatia wasi wasi kutokana na sababu kwamba ugonjwa huo unaripotiwa kwenye maeneo makubwa ambapo watu hawaelewi njia zozote za kuuzuia na kuutibu ugonjwa huo.

Mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa likiweno la kuwahudumia watoto la UNICEF yanatoa bidhaa za matibabu pamoja na hamasisho kwa jamii. Marixie Mercado ni kutoka UNICEF.