Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia nchini Liberia wapiga kura

Raia nchini Liberia wapiga kura

Raia nchini Liberia hii leo wamepiga kura kwenye uchaguzi wa urais na ubunge, uchaguzi unaoonekana kama kiungo muhimu katika kudumisha amani na demokrasia nchini Liberia . Hii ndiyo mara ya kwanza Liberia inajisimamia na kujiendelezea uchaguzi baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 kusimamiwa na Umoja wa Mataifa.

Wagombea 16 akiwemo rais Ellen Johnson Sirleaf wanawawania urais. Msemaji wa ujumbe wa UM nchini Liberia UNMIL Yasmina Bouziane anasema kuwa UNMIL imesambaza wanajeshi ili kuimarisha usalama nchini humo wakati wa kura hiyo.